Friday 31 January 2025 - 11:42
Kiongozi Muadhamu atoa heshima kwa Imam Khomeini na mashahidi wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, alitembelea makaburi ya Imam Khomeini (RA) na mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu leo Alhamisi asubuhi.

Kiongozi Muadhamu  atoa Heshima kwa Imam Khomeini na Mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Ziara hiyo ilifanyika kabla ya maadhimisho ya Siku Kumi za Fajr (Al-Fajr), ambazo huadhimisha kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ya mwaka 1979.

Kiongozi huyo alisali  na kusoma Qur’an, akitoa heshima kwa muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, marehemu Imam Khomeini.

Ayatollah Khamenei pia,  alitembelea makaburi ya mashahidi kadhaa wa Mapinduzi ya Kiislamu, wakiwemo Ayatollah Seyed Mohammad Beheshti, Mohammad Ali Rajaei, na Mohammad Javad Bahonar, katika makaburi ya Behesht Zahra (SA) kusini mwa Tehran.

Kiongozi huyo alitoa heshima kwa mashahidi na kuwaombea daraja za juu katika maisha ya milele.

Kila mwaka, mamilioni ya Wairani kote nchini huadhimisha siku kumi za sherehe kuadhimisha kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979, ambayo yaliuangusha utawala wa kifalme wa Pahlavi uliokuwa ukiungwa mkono na Marekani.

Siku ya kurejea kwa Imam Khomeini (Februari 1 mwaka huu) inaashiria mwanzo wa Siku Kumi za Fajr (Siku Kumi za Alfajiri), ambazo hufikia kilele chake kwa maandamano ya kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mnamo Februari 11.

Zaidi ya Matukio 10,000 ya Qur’ani Tukufu  yamepangwa kwa Kumbukumbu ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Taifa la Iran lilipindua utawala wa kifalme wa Pahlavi ulioungwa mkono na Marekani miaka 45 iliyopita, likihitimisha utawala wa kifalme wa miaka 2,500 nchini humo.

Mapinduzi ya Kiislamu yaliyoongozwa na marehemu Imam Khomeini (RA)  yaliunda mfumo mpya wa kisiasa uliozingatia maadili ya Kiislamu na demokrasia.

Chanzo: IQNA

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha